Muziki wa kizazi cha kale ‘Zilizopendwa’ umepata pigo kubwa baada ya mmoja wa magwiji kuondoka kwenye sura ya dunia.

Msanii huyo mkongwe mkali wa nyimbo kibao ikiwemo ‘Sasa Ni Lunch Time’ amefariki dunia hii leo alfajiri kwenye hospitali Moja ya rufaa maeneo ya Busia nchini Kenya akiwa na umri wa miaka 80.

Gabriel Omolo

Gabriel Omollo anasemekana kuugua homa ya mapafu ambayo imesababisha kifo chake.
Wengi wamemfahamu kwa tungo zake kali japo kizazi cha ‘ Shisha’ na ‘Internet’ sio wengi wamekuwa wakimfahamu. Mola ndiye atoaye na ndiye atwaaye, jina lake liimidiwe. 

Makiwa ndugu na jamaa za mwenda zake Gabriel Omollo.

#Mitego EA

Leave a Coment