Rais wa WCB, Diamond Platnumz ametangaza
habari njema kwa watanzania hasa hasa kwa
wadau wa tasnia ya habari kwamba anatarajia
kufungua Wasafi FM na Wasafi TV.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na
wimbo ‘Waka’ akiwa amemshirikisha msanii wa
muziki wa kufoka kutoka Marekani, Rick Ross,
alitoa taarifa ya ujio wa redio hiyo na TV kupitia
twitter yake Disemba 30 mwaka 2017 lakini
muda mfupi baadae aliifuta taarifa hiyo.

Screen-Shot-2018-01-06-at-12.36.16

Weekend iliyopita muimbaji huyo akiwa nchini
Kenya katika show za kuufungua mwaka 2018
alifanya mahojiano na kituo cha runinga cha
KTN/Citizen 10/10/K24TV na kueleza mpango wake huo wa kufungua
Wasafi FM na Wasafi TV.

Screen-Shot-2018-01-06-at-12.35.32.png

Hiyo ni habari njema kwa wadau wa habari
kwani kuanzisha kwa kituo hicho bila shaka
kitazalisha ajira za kutosha kwa watanzania.

Leave a Coment