Muziki kama madini una chimbuko lake sehemu fulani kwenye jamii fulani.

Wasanii wengi wameshaimba kwenye mitindo mbalimbali ya sanaa ya muziki bila kufahamu asili ya muziki huo.

Muziki kama Reggae, Ragga, Rhumba, Hip Hop, Genge, Ghipuka, Bongo Fleva na kadhalika zimechipukia Afrika na zinapigwa humu barani.

Skani

Bongo Fleva kwa mujibu wa msanii mmoja matata kutokea Pwani ya Kenya, ameeleza wazi chimbuko lake wakati akiwa kwenye mahojiano na Mzazi Willy M Tuva kwenye 10/10 show ya Citizen TV kwa hisani ya Dickson,Ring Ring Entertainment.

Johnny Skani ambaye amekuwa kwenye tasnia zaidi ya miaka kumi, amefunguka kusema kuwa muziki wa bongo fleva ulianzishwa zamani Mombasa na msanii Malkia Rukia alipokuwa akiimba ngoma zake za Hip Hop Taarab lakini baadae ukafika kwenye studio za Bongo Records Tanzania wakati akirekod humo na hapo ukatambaa Tanzania.
#MitegoEA

Leave a Coment