Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Dah! Mwezi February unaanza kwa habari za tanzia kisa kifo cha star wa muziki Uganda.

Ni habari za kuhuzunisha kwa mashabiki na wadau wa muziki mzuri wa hip hop ragga na dancehall baada ya kumpoteza gwiji msanii aliyekuwa mtajika kwenye kundi la Good Lyfe.

Moses Sekibooga aka Radio ameripotiwa kufariki dunia hii leo tarehe mosi mwezi wa pili akiwa kwenye chumba cha watu mahututi ICU baada ya kuhusika ajali ya barabarani na gari lake mnamo tarehe 28 January 2018.

Mkali huyo aliunda kundi lao ‘Good Lyfe’ pamoja na mwenzake mdogo wa super star lengend Joseph Mayanja ‘Chameleone’ ambaye ni Weasel.

Radio amefahamika kupitia nyimbo nyingi zake kali kama vile ‘Zuena, Don’t Cry’ ft Wizkid na nyinginezo nyingi.

Itakumbukwa kuwa rais wa Uganda Yoweri Museveni alikuwa ametoa kima cha pesa milioni kumi (10M) za Uganda kumgharamia matibabu msanii huyo mwenda zake.

Radio

Mitego Sasa inawapa pole ndugu , jamaa na marafiki pamoja na mashabiki kwa ujumla.

#MitegoEA

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.

Leave a Reply