Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Dah! Balaa lanuka kweli kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kukamatwa kwa wacheza muziki vilabu yaani Djs.

Baada ya kukamatwa kwa Dj wa gospel music, Dj MO mtindo huo wa kihuni wa watu wanaojidai ni maafisa wa halmashauri ya kuthibiti na kulinda mazingira NEMA, wakenya wamecharuka kufuatia tabia hio ya wizi wa kuaminika.

DJ Mo akiwa chini ya maafisa hao

Wengi wa madjs wamekamatwa vilabu wakiwa kazini kutumbuiza na kuchangamsha customers wa clubs kwa madai ya kupiga kelele usiku huku wakitozwa faini kubwa kati ya Ksh. 30,000-150,000 na vitishio vya kuwekwa rumande kama hamna faini.

Wakenya na watu maarufu kama Sauti Sol, Dj Joe Mfalme, Kriss Darling, Wyre na mastaa wengi wamekemea uhuni huo vikali kwa kuwataka waachilie MaDjs na kufanya kazi yao ya kupambana na wezi mitaani sio kuingilia kupora wakenya wasiona hatia.

Hata hivyo wametoa wito kwa viongozi haswa wa kaunti ya Nairobi kuingilia kati ujambazi huo unaoendeshwa kwa sasa.

#MitegoEA

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.

Leave a Reply