in

Diamond Platnumz Aingia Studio Na Rihanna, Itakuwaje!πŸ’₯πŸ‡ΉπŸ‡Ώ

Jamanii Simba amegoma kurudi nyumbani baada ya kuangukia pua tuzo za BET Marekani.

Wengi wa mashabiki wa Diamond Platnumz wanasema kuwa msanii huyo huenda akawa anaona aibu kurudi nyumbani Tanzania baada ya kuambulia patupu tuzo za BET zilizofanyika huko Marekani mwishoni mwa mwezi Juni.

Diamond Platnumz alishindwa na msanii Burna Boy aliyetuzwa kama ‘Best International Act’.

Mashabiki wanadai kuwa Simba anawazuga kwa kujifanya kuwa yuko Marekani kwa ajili ya maandalizi ya Album yake mpya ‘World Album’ itakayoshirikisha mastaa wakubwa wa muziki duniani.

Licha ya madai hayo, msanii huyo wa bongo fleva amekuwa akitupia picha mbalimbali akiwa na wasanii wakubwa kama vile, Bustar Rythmes, Hitmaka, The Real Swizz, Wizkhalifa lakini pia anadaiwa kuingia studioni na Rihanna. Je, itakuwaje?

Je ni kweli Diamond Platnumz anaogopa aibu kurudi nyumbani Tanzania au yuko busy akiandaa Album?πŸ€”πŸ‡ΉπŸ‡Ώ

What do you think?

Written by Antony Makenzi

Antony Makenzi is a content writer who has sharpened his skills and absorbed knowledge on Financial freedom, Wealth, Making Money Online and development of a mindset!

Comments

Leave a Reply

Loading…

0

Nay Wa Mitego ‘Amvua Nguo Tajiri Fred Vunja Bei Kisa Ushamba’ πŸ™ŠπŸ€£πŸ‡ΉπŸ‡Ώ

Michael Jackson New Music And Albums, Confirms His Former Bodyguard Matt!πŸ”₯πŸ’ͺ🏼