Msanii Ali Kiba maarufu kama King Kiba amefunguka kuhusu chanjo cha mapato na utajiri wake mnono.
King ameeeleza kupitia account zake za social media kuhusu maisha yake ya muziki lakini pia private life yake ya biashara za kilimo haswa upanzi wa Nyanya.

Hii hapa kauli yake full;
“Wengi wanaonifahamu wamenifahamu kupitia muziki wangu. Hii haijatokea kwa bahati mbaya coz maisha yangu nje ya muziki kwa kiasi kikubwa niliamua kuyaacha yawe private.
•
Kwa muda mrefu nimewekeza kwenye kilimo na kiukweli imekuwa experience ya tofauti iliyojaa changamoto lakini yenye mkwanja kinoma. Nimesukumwa sana ku-share hii na vijana wenzangu ili kuunga Mkono jitihada za Bi. Mkubwa kwa Vijana wenzangu sababu nakiona Kilimo kuwa ni kitu cha uhakika kinachoweza kubadili life yetu.
Wanasema ukitaka mali utaipata shambani, mimi nakwambia ukitaka mkwanja jitupie kwenye kilimo. Kila nikipata time nitakuwa na-share hapa challenges zangu kwenye kilimo na mikwanja ambayo nimeiokota huko.” Yeye kamaliza hivyo!
Je una maoni gani kuhusu biashara yake ya kilimo?



GIPHY App Key not set. Please check settings