in

Harmonize Amvamia Ali Kiba Kwenye Interview Balaa Kubwaa! 😫

Je Mbona Harmonize amemvamia msanii Ali Kiba Kwenye show?

Je kuna bifu au ndio mwanzo wa ushikaji kati yao wawili?

Harmonize ameonekana kushow love Kwa Msanii Ali Kiba wakati Wapo Kwenye event ya Rais Mama Samia Suluhu Hassan huko Zanzibar.

Licha ya kuwa Tamasha la rais, wasanii walikuwa wamealikwa kama vile Ali Kiba, Zuchu, Harmonize, Mwijaku, Baba Levo, Shoro Mwamba na wengineo.

Harmonize na Ali Kiba kwenye Ndege na pia Ali Kiba alikumbatiwa na Harmonize Zanzibar.

Harmonize aka Tembo aliforce tukio kubwa baada ya kumtokea kwa nyuma Ali Kiba akiwa live Kwenye interview na kumkumbatia kama rafiki wake. Japo wawili hao hawajawahi kukaribiana Kwa sana hivyo mbali na tukio la msiba Video vixen Agnes Masogange wapokutana live, Ali Kiba, Harmonize na Diamond Platnumz wakati Wapo Wasafi Classic.

Tukio lingine ni pale walikutana Kwenye Ndege kwenye safari moja na wakakaa karibu wakipiga story.

Harmonize baada ya kuondoka Wasafi WCB amekuwa na bifu na Ex Boss wake Diamond Platnumz na kuonekana mnafiki kwani ameshow love mpinzani wake Diamond Platnumz- Ali Kiba.

Mara baada ya tukio hilo Mwijaku na watu wengine walifurahi wakashangilia wakisema Familia imekutana. Harmonize alitoa kauli akasema kuwa Ali Kiba ndiye King wa Muziki Tanzania. Je ni kweli?

Ali Kiba akiwa live Kwenye Interview avamiwa na Konde Boy Harmonize

Je Harmonize Na Ali Kiba wanaungana kumpoteza ‘Simba’ Diamond Platnumz Kwenye muziki wataweza?

Hii hapa video ya tukio hilo huko Zanzibar . Tazama!

What do you think?

Written by Antony Mckenzy

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GIPHY App Key not set. Please check settings

Ommy Dimpoz Na Diamond Platnumz Tena New Collabo! 🎧🔥

‘Toto La South Sudan’ – John Frog ft Bahati (Official Music Video)