in ,

MWILI WA JEFF MWATHI WAFUKULIWA TENA! 💀⚰️😭

Kufuatia kifo tatamishi cha Jeff Mwathi, police wa kitengo cha Upelelezi (DCI) eneo la Rift Valley wameongoza zoezi la ufukuzi wa mwili Hii Leo.

Jeff alifariki dunia kwa namna isiyoweza kuelezeka na kuzikwa kwa haraka sana kabla ya kubainisha kifo chake.

Inadaiwa kuwa alikumbana na umauti wake baada ya kuhudhuria hafla kwa DJ Fatxo.

Hata hivyo DJ Fatxo amekuwa miongoni mwa washukiwa wakuu wa mauwaji ya Jeff Mwathi japo bado hajatiwa mbaroni kwa uchunguzi zaidi. Kisa hiki kiligadhabisha wafuasi na mashabiki lakini pia familia ya marehemu Jeff Mwathi.

Dj Fatxo na Jeff Mwathi

Leo hii mwili wake unafukuliwa katika kaburi huko Nakuru ili upasuaji ufanyike kubainisha kilichosababisha kifo chake cha gafla.

Zoezi nzima la ufukuzi limechukua masaa matatu kwani inafaa kufanyika taratibu kwenye uchimbaji wa Kaburi ili pasitokee hitilafu kwenye mwili wake kitu ambacho kinaweza kuchangia kupata matokeo mabovu kama watagusa geneza au mwili wake Kwa Jembe kwa mujibu wa Mkuu Wa Kitengo cha upelelezi eneo la Rift Valley.

What do you think?

Written by Antony Mckenzy

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GIPHY App Key not set. Please check settings

“SOKO NI CHAFU” OKERE BLACK WARNS DIANA B! 😤

<Forever > ~ Rayvanny (Official Music Video)