Je unasubiri hii bonge la collabo kutoka Kwa hawa washikaji wa kutoka jadi?
Na je nini kilikiwa chanzo cha ugomvi kati ya Ommy Dimpoz na Diamond Platnumz aka Simba?
Wawili hao ni wasanii wakali wa Bongo Fleva Tanzania lakini pia ni marafiki wakubwa licha utofauti uliojitokeza wakatengana.

Kwenye mojawapo ya interviews za radio Tanzania, The Switch show – Wasafi Tv , Ommy Dimpoz ameweka wazi kuwa yeye na Diamond walitofautiana kwenye suala la muziki kwani yeye alikuwa akimsapoti msanii Ali Kiba ambaye ni mpinzani wa Diamond Platnumz Kwenye Muziki.
“Utimu ndio chanzo kikubwa kwani mimi na Ali Kiba ni washikaji so Platnumz hakulichukulia Poa suala hilo kwani pia ana timu yake. Lakini tumekuwa tukizungimza Kwenye moments tofauti we meet off cameras we talk. Sisi tukaamua kumaliza Bifu zetu na tunafocus sana na Maisha haswa biashara kwani tushakua na tumekomaa” Ommy azungumza.
Je baada ya kumaliza utofauti wao tutegemee nini kutoka kwao tena kwani pia Wana history kubwa ya kufanya collabo kalii kali enzi zao !?
GIPHY App Key not set. Please check settings