in

Sababu Kubwa Ya Diamond Karanga Kupigwa Marufuku! 😫

Hii nayo ni Balaa nzito sana kwani Diamond Karanga zilikuwa habari ya mjini kabla ya kupigwa marufuku.

Kwa sasa bidhaa maarufu ya ‘Diamond Karanga’ haipo tena sokoni. Hii inafuatia baada ya kuvunjika Kwa makubaliano baina ya Diamond Platnumz na Wasafi Media dhidi ya kampuni ya Smart Industry Limited’ambayo ndio watengenezaji Wa hio bidhaa.

Kuwa Wa Kwanza Kutangaza Biashara au Bidhaa yako Kwa Watu Wote Duniani Kupitia Mitego Sasa website. Tupigie Simu Leo kupata Hii Nafasi Kubwaa Zaidi; +254702662012

Baada ya kuzuka Kwa Kutoelewana kibiashara kati ya Wasafi Media na Smart Industry Limited, Diamond Platnumz aliishia kushtaki Smart Industry Kwa kutumia kina lake ‘Diamond’ kwenye bidhaa hio lakini pia hasara ya kufanya matangazo ya hio bidhaa ya Diamond Karanga’.

Kesi ilikuwa moja nzito kwani pia Smart Industry walijibu mapigo hayo ya Diamond Platnumz kudai mamilioni ya pesa kama fidia lakini kesi yao ikabidi wasuluhishe nje ya korti na kumaliza mzozo wao, kwani Smart Industry Limited walitaka Diamond Platnumz Pamoja Joseph Kusaga kulipa fidia Kwa Smart Industry Limited kwani wao walisababishia hasara kampuni hio baada ya kugoma kufanya matangazo ya bidhaa hio kama ilivyokuwa Kwenye contract ya kakubaliano.

Simba na Smart Industry Limited wakamaliza kesi yao bila korti kuhusishwa, sasa kesi ikamlalia Joseph Kusaga ambaye yeye hakujitetea hata mbele ya mahakama after kesi dhidi yao Pamoja na Diamond Platnumz kuwasilishwa kortini.

Lakini korti imeamua kutupilia mbali ombi la Smart Industry Limited dhidi ya Kusaga kwani hakuna vile anaweza kulipia fidia ya matangazo ya bidhaa hio pekee wakati mwenzake ‘Diamond’ ambaye wasaini pamoja mkataba Wa mauzo alishaachiliwa huru na Smart Industry Limited.

Hivyo, korti imeamshauri Smart industry kufanya kufungua kesi nyingine upya dhidi ya Kusaga iwapo wanadai kupata fidia kutoka kwake.

Tazama hii video hapa ili kupata maelezo zaidi kuhusu Kisa cha kesi ya ‘Diamond Karanga’

Je, Ulipenda Diamond Karanga? Na Kwa Nini ?

What do you think?

Written by Antony Mckenzy

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GIPHY App Key not set. Please check settings

Motra The Future – Arap Moi Jr (Official Audio)

‘Naringa’ – Zuchu (Official Music) New Download!👌