Hivi ndio dunia imekengeuka au ndio wasanii wetu wameweuka?
Muziki wa kisasa umekuwa kama mashindano ya mwonekano wala sio Muziki.

Ukishangaa ya Konde Boy aka Harmonize, hujayaona ya Simba Diamond Platnumz.
Simba ametupia baadhi ya picha akiwa nchini Afrika Kusini huku akiwa kwenye studio.

Mkali huyo wa bongo fleva Tanzania na duniani Kwa sasa ameonesha mtindo mpya wa vazi la viatu vya aina yake vyenye saa ya mkononi kwenye sura ya mbele ya Viatu.

Baada ya Harmonize kuibuka na ‘Altitude’ wimbo uliovunja rekodi kwenye mitandao kwani video yake alionyesha vazi kali lenye ‘Vijiko, Uma, Visu’ kama fesheni mpya ya Sanaa ya sasa.

Hapa naye Diamond Platnumz akiwa tayari kuachia album yake ya nne ya muziki, naye ametupia picha hio yenye fasheni mpya ya viatu.

Je, unadhani Muziki ni Mwonekano au ni kuelimisha jamii?